Usanii wa Nanqu licha ya kuvutia kwa sauti yake, lugha inayotumika pia ni ya kifasihi. Ufuatao ni ubeti mmoja unaoimbwa, ukisema,
"Majira ya mchipuko yamepita, yafuatayo ni majira ya joto, na punde si punde yatakuja majira ya mpukutiko. Kwenye mto ndani ya msitu mashua imetulia, mvuvi alisimama kwenye ncha ya mashua akirusha nyavu ."
Kwa kawaida usanii wa Nanqu huoneshwa na mtu mmoja akiwa amekaa anaimba huku akipiga kinanda mwenyewe, lakini kwa mujibu wa mambo yanayoelezwa pia Usanii wa Nanqu huoneshwa na watu kadhaa wakiimba huku wakipiga vinanda.
Wimbo huu unaendelea kusema, "Samaki wavuliwa, wasiwasi wanitoka. Pombe yanilevya, sijali majira yakipita."
Kwa maneno machache wimbo huo umeeleza vilivyo jinsi wenyeji wa huko wa kabila la Watujia wanavyofurahia maisha wakiwa katika mazingira mazuri yenye milima na mito. Katika maisha ya Watujia, Nanqu ni mchezo wa sanaa wasiyoweza kutengana nayo kwani inawapa furaha kila siku.
Usanii wa Nanqu una aina nyingi tofauti ambazo baadhi yao ni za furaha na nyingine ni za huzuni. Lakini aina zote hizo haziwezi kuachana na ala ya muziki iitwayo Sanxian kwa Kichina, hiki ni kinanda chenye mpini mrefu uliofungwa nyuzi tatu, eneo la sauti yake ni kubwa kutoka juu mpaka chini.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |