"Upepo wapukutisha majani, maua yanukia kila mahali. Katika usiku huu tulivu ni nani anayepiga kinanda kama kishindo cha chuma?"
Wimbo huu unaeleza masikitiko katika majira ya mpukutiko wa majani. Michezo ya sanaa ya Nanqu licha ya kupatikana kutoka katika riwaya maarufu za kale kama "Madola Matatu ya Kifalme", "Mashujaa kwenye Vinamasi" na "Hadithi za mapenzi katika Chumba cha Magharibi", pia inapatikana kutokana na mila na desturi za Watujia kama vile "Mama Mnene Avuka Mto" na "Kivunjajungu Ataka Mke".
Hivi sasa Usanii wa Nanqu wa jadi umewekwa kwenye orodha ya urithi wa utamaduni usioonekana wilayani humo na inatunzwa na serikali, mpaka sasa kuna warithi wa utamaduni huo zaidi ya mia moja. Usanii wa Nanqu umepata nguvu ya kuendelea kustawi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |