• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Upendo kwa watoto wenye ugonjwa wa mifupa ambayo ni rahisi kuvunjika

    (GMT+08:00) 2009-11-10 20:18:15

    Katika jengo moja lililoko eneo la Xuanwu mjini Beijing, kuna shirika moja maalumu la kiraia linaloitwa shirika la upendo kwa watoto wenye ugonjwa wa mifupa yenye hatari ya kuvunjika, ugonjwa huo kitaaluma unaitwa 'Osteopsathyrosis', watoto wenye ugonjwa huo si kama tu huwa ni wafupi na wadogo sana, bali pia mifupa yao ni miepesi na ni rahisi kuvunjika kama vyombo vya kauri. Hivi sasa kuna wagonjwa laki moja hivi wa ugonjwa huo nchini China.

    Katika ofisi ndogo ya shirika hilo, mwandishi wetu wa habari alikutana na mwanzilishi wa shirika hilo Bi. Wang Yiou. Msichana huyo anaonekanani mdogo sana na urefu wake ni mita moja tu, macho yake ya rangi ya kibuluu yalikuwa yanang'ara chini ya nywele zake zilizojisokotasokota.

    Mwandishi: unaonekana kama mwanasesere, wala si mtoto wa sanamu ya kauri.

    Wang: macho yangu yanaonekana ni rangi ya kibuluu, ambayo ni dalili ya ugonjwa huo.

    Alipokuwa mtoto Wang Yiou alisumbuliwa mara kwa mara na kuvunjika kwa mifupa na alilazimika kuacha shule, lakini tatizo la ugonjwa wake bado ni dogo ikilinganishwa na hali ya wagonjwa wengine. Wang Yiou alisema:

    'Tangu nilipozaliwa hadi nilipofikia umri wa miaka 16 nilivunjika mifupa mara 6, idadi ambayo ni ndogo sana kuliko wagonjwa wengine. Wengi wao wenye ugonjwa huu ninaowafahamu walivunjika mifupa mara kumi kadhaa na hata hadi zaidi ya mara mia moja, kwa mfano katika siku ya pili tangu alipozaliwa, alivunjika mifupa mara mama yake alipomkumbatia.'

    Kutokana na bidii zake kubwa na kuchukua tahadhari kwa makini zaidi, msichana huyo anayependa kucheka aliandikishwa na chuo kikuu cha mawasiliano cha Beijing. Aliposoma katika chuo kikuu hicho, alifahamu kwamba kuna watu wengi wenye ugonjwa huo nchini China, kwa hiyo alianzisha tovuti yenye jina la 'mji wa vioo' kwenye mtandao wa Intenet, ili kutoa taarifa za matibabu kwa watu wenye ugonjwa huo na kutoa misaada kwa wagonjwa wanaokuja Beijing kupata matibabu.


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako