Katika pilikapilika hizo Bi. Wang Yiou alipita muda wake wa chuo kikuu. Wakati wa kuhitimu alipata shahada mbili za kwanza za masomo ya uhasibu na sheria, na alipata ajira nzuri katika idara moja ya sheria, ambayo ni muhimu sana kwa msichana huyo mwenye ugonjwa huo wa mifupa. Lakini baada ya mwaka mmoja tu, alijiuzulu kazi hiyo. Wang Yiou alisema, alikuwa anataka kuanzisha shirika la kutoa misaada kwa watu wenye ugonjwa huo wa mifupa. Bi. Wang Yiou alisema:
"hata sikuthubutu kuwaambia wazazi wangu kwamba nilijiuzulu kazi yangu. Baada ya miezi mitatu nilifikiri kwamba siwezi kuficha siku zote, kwa hiyo nilimwambia mama yangu, lakini jibu la mama yangu lilinishangaza sana. Aliniambia kwamba ulivyosema ni vizuri, kama kuungekuwa na shirika kama hilo wakati ulipokuwa mtoto, basi tusingekata tamaa na kupoteza matumaini kama tulivyokuwa. Tunakuunga mkono kwa nguvu yote, kuwa mmoja wa watu wanaojitolea."
Kwa hiyo shirika la kutoa misaada kwa watu wenye ugonjwa huo wa mifupa lilianzishwa rasmi, na mwanzoni lilikuwa na wafanyakazi wawili tu, Bi. Wang Yiou na Bw. Huang Rufang. Kijana huyo alipatwa ugonjwa mwingine wa ukuaji wa mifupa, urefu wake unafanana na Bi. Wang Yiou na uzito wa jumla wa hao wawili haufikii kilo 50, lakini ni watu hao wawili waliobeba matumaini ya watu wengi wenye ugonjwa huo.
Msichana huyo mwenye umri wa miaka 20 tu ana nguvu kubwa ya kuhimili ugonjwa ambayo hata watu wa kawaida hawawezi kufikiria, kamwe hakulia kutokana na maumivu, lakini siku moja alilia sana barabarani kutokana na matatizo aliyopata kwenye shughuli za kuchangisha fedha kwa ajili ya shirika hilo, wakati huo Wang Yiou na shirika lake hakuweza kumudu hata kodi ya ofisi. Wang Yiou alisema:
"Nilikuwa nimekataliwa na shirika moja la mfuko, halafu nilipigiwa simu moja, ambapo mzazi mmoja wa watoto akilia aliniambia kwamba mtoto wake alivunjika mifupa tena, lakini hana pesa za kumfanyia oparesheni. Wakati huo niliona siwezi kuwasaidia hata kidogo, ingawa nilianzisha shirika hilo, lakini wakati wanapohitaji kabisa misaada, sikuweza kuwaambia kwamba basi njoo tunaweza kukupatia matibabu, wakati huo hatukuweza kuahidi namna hiyo."
Wakati huo mzee Wan alijitokeza na kumsaidia Wang Yiou kupita kwenye wakati mgumu. Huyo mzee alikuja Beijing kutoka mkoa wa Zhejiang. Alipoona Wang Yiou anafanya kazi katika ofisi mbovu na hata hawakuweza kutoa mishahara kwa wafanyakazi, aliamua mara moja kutoa misaada ya fedha kwa shirika hilo. Mzee Wan ni mfanyabiashara, mwanzoni alitaka kutoa yuan elfu 50, halafu aliona kwamba pesa hizo hazitoshi, siku iliyofuata alitoa yuan laki moja kwa shirika la Wang Yiou.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |