• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Upendo kwa watoto wenye ugonjwa wa mifupa ambayo ni rahisi kuvunjika

    (GMT+08:00) 2009-11-10 20:18:15

    Bi. Wang Yiou alisema, sasa matumaini yake makubwa ni kuweza kuihimiza China iweke sheria husika ya kulinda maslahi ya watu wenye ugonjwa huo wa mifupa na magonjwa mengine ambayo ni nadra kutokea. Baada ya kutumiza matumaini hayo, Wang Yiou alisema ataishi maisha yake kama anavyopenda. Alisema:

    "kama siku moja matatizo yanayokabili kundi la watu wenye ugonjwa huo yatakuwa yametatuliwa, nitarejea kwenye kazi zinazohusu mambo ya sheria. Nitaishi maisha yangu kwa ninavyopenda, nitakuwa na nafasi za kusikiliza nyimbo, kutazama filamu na kufanya mambo mengine mengi ninayopenda."

    Tunaweza kusema kwamba njia inayoelekea kutimiza matumaini ya Wang Yiou imeonekana kuwa na mustakabali mzuri. Kama tukisema shirika lililoanzishwa na Wang Yiou na mashirika mengine ya kutoa misaada kwa watu wenye magonjwa magumu ni kutoa fursa kwa wagonjwa, basi hivi sasa watu wengi zaidi wamejaribu kusukuma mbele ujenzi wa mfumo wa taifa kuhusu mambo hayo kwa njia yenye ufanisi zaidi. Baadhi ya wajumbe wa taifa walitoa mara nyingi mapendekezo ya kulinda maslahi ya watu wenye magonjwa ambayo ni nadra kutokea kwenye mkutano mkuu wa bunge la umma la China. Mswada kuhusu sheria ya kinga na udhibiti wa magonjwa adimu ulichukuliwa na halmashauri ya kudumu la bunge la umma la China na hivi sasa umeingia kwenye kipindi cha utungaji wa sheria. Hali hiyo si kama tu imewapa upendo watu wenye mgonjwa adimu ambayo ni nadra kutokea, na bali pia imewatia matumaini, imani na nguvu.


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako