• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nyumba ya Lu mjini Shaoxing yenye umaalum

    (GMT+08:00) 2009-11-16 15:42:56

    Mji wa Shaoxing, mkoani Zhejiang kuna kundi moja la majengo ya enzi ya Ming, ambayo yalikuwa nyumbani kwa ofisa mmoja wa zama za kale, na ni nadra kuonekana kwenye sehemu ya kusini mwa China. Majengo hayo ya taadhima, yalijengwa kwenye mistari mitatu kutoka chini kwenda juu na kwenye mistari mitano ya kutoka kushoto kwenda kulia, na kuwa katika sehemu 13, ambazo kila moja imezungushiwa kwa ukuta mkubwa. Wasomi mashuhuri wanasifu kuwa, "kwenye sehemu ya kaskazini kuna majumba ya wafalme wa zamani, na kwenye sehemu ya kusini kuna Nyumba ya Lu".

    Nyumba ya Lu iko kwenye upande wa ndani wa kichochoro mjini Shaoxing, eneo la majengo hayo ya makazi ni mita za mraba zaidi ya elfu 32. Fremu ya mlango ya mawe, mlango mkubwa wa rangi nyeusi, kuta za rangi nyeupe, vigae vya rangi ya kijivu kwenye mapaa ya nyumba, yote hayo yanafanya majengo ya nyumba hiyo kuwa ya taadhima na nadhifu sana, Nyumba ya Lu ni mfano wa majengo yenye ua ya jadi kwenye sehemu ya kusini ya China.

    Ukumbi wa Yong'en ni jengo ambalo limehifadhiwa vizuri zaidi katika Nyumba ya Lu. Ukumbi wa Yong'en ni alama ya majengo ya Nyumba ya Lu, vilevile ni ukumbi mkubwa kabisa kati ya kumbi 13 kwenye Nyumba ya Lu. Ufahari ya ukumbi wa Yong'en unaonesha ufahari wa Nyumba ya Lu wa miaka ile ya zamani. Ukumbi wa Yong'en una kimo cha mita 8.5, urefu wa mita 17 na upana wa mita 6.5. Nguzo za ukumbi huu ni magogo, ambazo watu wawili wakishikana wanaweza kuizungushia mikono nguzo hiyo. Michoro ya rangi iliyoko kwenye maboriti ya ukumbini bado inaonekana. Chumba kilichoko kwenye sehemu ya kati ya ukumbi huu kinaitwa Mingtang, ambacho ni kikubwa zaidi. Mtaalamu wa historia wa huko Bw He Xinen alisema,

    "Nyumba ya Lu vilevile inaitwa "kumbi 13 za Nyumba ya Lu, ambalo lilijengwa katika enzi ya Ming ya mfalme Jia Jing kati ya mwaka 1549 na 1583. Nyumba hiyo ilikuwa ni ya Lu Tao, katibu wa mfalme na mwalimu wa mtoto wa mfalme wa enzi ya Ming, ambayo ni kubwa na nadra kuonekana kwenye sehemu ya kusini ya China. Lu Tao alipendwa na mfalme Jia Jing kutokana na taarifa moja aliyomwandikia mwaka 1532 alipokuwa na umri wa miaka 46, na tokea hapo alipandishwa cheo moja kwa moja hadi kuwa katibu wa mfalme na mwalimu wa mtoto wa kwanza wa mfalme kwa zaidi ya miaka 10, cheo chake hicho kilikuwa cha ngazi ya kwanza kwa maofisa wa enzi ya kifalme".


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako