• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nyumba ya Lu mjini Shaoxing yenye umaalum

    (GMT+08:00) 2009-11-16 15:42:56

    Moja ya jadi za wakazi wa mji wa Shaoxing ni kujenga nyumba nzuri, ambayo inaonesha ufahari wa familia, hali ya nyumba inaonesha hadhi ya ukoo wake. Katika historia ya mji wa Shaoxing, wamewahi kujitokeza watu wengi mashuhuri, lakini maofisa walioweza kupata wadhifa wa juu kama wa Lu Tao walikuwa wachache sana, kwa hiyo kumbi 13 kwenye Nyumba ya Lu zilijengwa kwa ufahari na taadhima.

    Inasemekana kuwa, kumbi 13 kwenye Nyumba ya Lu zilikuwa zawadi iliyotolewa na wanafunzi wake 13 wa zamani wakati waziri wa elimu Bw Lu alipotimiza umri wa miaka 80. Mtaalamu wa idara ya mabaki ya utamaduni ya mji wa Shaoxing Bw Fu Jianhua alisema,

    "Kumbi 13 za Nyumba ya Lu zilijengwa na wanafunzi wake, kila mwanafunzi alijenga ukumbi mmoja. Msomi aliyepata mafanikio ya kuchukua nafasi ya kwanza katika mtihani mkuu, alichukuliwa kama ni mwanafunzi wake kwa muda fulani, hivyo baada ya waziri Lu kustaafu, kila mwanafunzi wake alimjengea ukumbi mmoja."

    Kama mtu akipanda ngazi na kuingia kwenye Nyumba ya Lu, nyumba zimetenganishwa kwa njia mbili za maji, moja inakwenda juu kutoka chini na nyingine inakwenda kulia kutoka kushoto, na kukutana kwenye sehemu ya katikati. Lengo la kujenga njia hizi lilikuwa ni kuzuia ajali ya moto, kuzuia wezi na kurahisisha mawasiliano. Baada ya kujengwa kwa njia ya pili ambayo ni pana zaidi inayokwenda kulia kutoka kushoto kwenye sehemu ulipo ukumbi wa Yong'en, wapanda farasi wanaweza kukimbia na farasi kwenye njia hiyo.


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako