• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nyumba ya Lu mjini Shaoxing yenye umaalum

    (GMT+08:00) 2009-11-16 15:42:56

    Lu Tao aliishi katika kipindi cha mwisho cha enzi ya Ming, ambayo ilianguka miaka 40 baada ya yeye kufariki dunia. Katika enzi ya Qing iliyofuata enzi ya Ming, hakukuwa na mtu wa ukoo huu aliyekuwa ofisa mkubwa. Hivyo baada ya muda Nyumba ya Lu iligawanywa kwa watu wa familia nyingine, na kuwa eneo kubwa kabisa la nyumba zinazokaliwa na watu wa familia mbalimbali mjini Shaoxing kwa wakati ule, huenda kutokana na kukaliwa na watu wa familia mbalimbali, nyumba za eneo hilo zilizojengwa katika enzi ya Ming ya zaidi ya miaka zaidi ya 400 iliyopita zimeweza kuhifadhiwa vizuri hadi sasa. Hivi sasa watu wa familia mia 3 au 4 hivi wanaishi kwenye nyumba hizo, na watu wa vizazi vya ukoo wa Lu wanaoishi huko wamekuwa wachache sana isipokuwa Bw Lu Dong. Bw Lu Dong alisema,

    "Nilizaliwa katika nyumba hiyo. Mimi ni kizazi cha 18 cha Lu Tao, na ni kaka mkubwa wa kizazi hicho. Mwaka huu nina umri wa miaka 86, ninajivunia sana kuweza kuishi hapa na kufanya kazi ya kuhifadhi nyumba za hapa, ningefurahi sana kama ningeweza kuishi hapa milele."

    Baada ya miaka mingi kupita, katika Nyumba ya Lu ambayo ni majengo ya kale yenye taadhima, majengo mengi yameharibiwa kwa kiasi tofauti. Mkurugenzi wa Idara ya mabaki ya kale ya utamaduni ya mji wa Shaoxing alisema, kuhifadhi Nyumba ya Lu ni kuenzi utamaduni wa majengo ya jadi ya China, hivi sasa tumechukua hatua kadha wa kadha za kuzuia majengo yasiendelee kuharibika, ili utamaduni wa majengo ya jadi ya China uoneshe mvuto wake wa kudumu.


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako