• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mabadiliko kwenye wilaya ya Mohe baada ya moto mkubwa ulioteketeza msitu

    (GMT+08:00) 2009-11-19 16:47:42

    Hifadhi ya mazingira ya asili ni jambo linalofuatiliwa sana kwa hivi sasa, na nchi mbalimbali zimepata fundisho kutokana na makosa ziliyofanya. Katika wilaya ya Mohe iliyoko kaskazini ya China, karibu na mpaka wa Russia, moto mkubwa ulitokea kwenye msitu wa wilaya hiyo miaka 22 iliyopita. Maafa hayo yaliteketeza msitu wa asili wa Daxing'anling, ambao ni mkubwa zaidi nchini China, na kuuteketeza kabisa mji wa wilaya ya Mohe. Baada ya maafa hayo, wilaya ya Mohe ilianza kutekeleza hatua za kuchukua tahadhari dhidi ya moto, kulinda maliasili ya misitu na kubadilisha mtizamo kuhusu kazi ya kujiendeleza. Hivi leo, misitu ya wilaya hiyo imezidi asilimia 90.

    Baada ya kuingia katika Jumba la makumbusho ya maafa makubwa ya moto ya misitu ya milima Daxing'anling wilayani Mohe, watu wanaweza kujionea hali ilivyokuwa wakati ule. Tarehe 6 Mei mwaka 1987, misitu ya Milima Daxing'anling ilikumbwa na moto mkubwa, ambao ulizimwa baada ya siku 28. Moto huo uliteketeza eneo la hekta milioni 1.01, na kusababisha vifo vya watu 211. Moto huo uliharibu vibaya mji wa wilaya ya Mohe na kusababisha hasara ya moja kwa moja yenye thamani ya zaidi ya Yuan milioni 500. Kazi ya ukarabati ikaanza kwa haraka, na wakati huohuo, watu walitambua kuwa, ni lazima kuhifadhi vizuri mazingira ya asili. Mwanzoni moto huo ulisababishwa na vitendo visivyofaa katika uzalishaji, hivyo wakazi wa huko pia walitambua kuwa shughuli za uchumi na uzalishaji ni lazima ziendane na uhifadhi wa mazingira ya asili.


    1 2 3 4
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako