• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mabadiliko kwenye wilaya ya Mohe baada ya moto mkubwa ulioteketeza msitu

    (GMT+08:00) 2009-11-19 16:47:42

    Ili kukumbuka maafa hayo, mwezi Oktoba mwaka 1988, Jumba la makumbusho ya maafa makubwa ya moto ya Milima Daxing'anling lilijengwa na kufunguliwa. Mkuu wa jumba hilo bibi Ma Yuanchun alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, lengo la kujenga jumba hilo ni kuwafanya watu wachukue tahadhari dhidi ya moto. Alisema,

    "Lengo kubwa la kujenga jumba hilo ni kuwaelimisha na kuwatahadharisha watu. Hivi sasa jumba hilo limekuwa kama ni kitabu cha elimu ya tahadhari dhidi ya moto wa misitu."

    Kila mwaka tarehe 6 Mei, shule za msingi na za sekondari za huko zinashirikisha wanafunzi kulitembelea jumba hilo, ili kuwafanya watoto hao wafahamu umuhimu wa hifadhi ya mazingira ya asili. Sasa miaka 22 imepita toka moto huo utokee, lakini watu wa Mohe bado hawajasahau fundisho lililotokana na moto huo.

    Karibu na jumba la makumbusho, kuna eneo kubwa la makazi la Yangguang. Kwenye eneo hilo la makazi kuna familia zaidi ya 3,500, ambazo zina watu zaidi ya 10,000. Mkurugenzi wa eneo hilo la makazi bibi Fang Hui alisema, kila mwaka inapofikia majira ya mchipuko na mpukutiko, watu wa sehemu hiyo wanatilia mkazo zaidi kazi ya kulinda usalama na kuchukua tahadhari dhidi ya moto. Alisema,

    "Kila majira ya mchipuko yanapofika tunatoa matangazo yanayohusu kujikinga dhidi ya maafa ya moto, na kukagua kazi ya kuchukua tahadhari dhidi ya moto kwa kila familia, ili wakazi watambue umuhimu wa tahadhari dhidi ya moto."


    1 2 3 4
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako