• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bw. Zhang Yong, balozi wa Urafiki kati ya China na Sudan

    (GMT+08:00) 2009-11-20 18:52:41

    Zhang Yong ni ofisa wa jeshi la China. Yeye alitumwa kwa mara mbili nchini Sudan kushiriki kwenye operesheni ya ulinzi wa amani ya Umoja wa Mataifa, ambapo aliwaongoza madaktari wanajeshi wa China kutoa matibabu kwa vipofu karibu 100, na kuwarudishia uwezo wa kuona. Kutokana na kazi yake kama hiyo, wenyeji Wasudan walimwita Zhang Yong "balozi aliyeleta mwanga", na kukisifu kikosi cha kulinda amani cha China nchini Sudan kwamba ni kikosi "kitakatifu".

    Mwaka 2005 kikosi alichokuwepo Zhang Yong kiliteuliwa kuwa kikosi kitakachotumwa nchini Sudan kushiriki kwenye operesheni ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa nchini humo. Bw. Zhang Yong alifurahia sana baada ya kupata habari hiyo. Amesema:

    "Mwanzoni mwa mwaka 2005, wakati nilipopata habari kuwa kikosi kinachoshughulikia kazi ya uchukuzi cha jeshi la kulinda amani kitaundwa na askari wa kikosi chetu, nilifurahi sana. Nilitoa ombi la kushiriki kwenye kikundi hicho mara moja, na kuomba mara kwa mara kuwa nataka kwenda Sudan kufanya kazi hiyo. Nilipoambiwa kuwa nimechaguliwa kuwa mmoja wa walinzi wa amani, hasa kwenye mkutano wa kuunda kikosi cha kulinda amani nchini Sudan uliofanyika tarehe 9 mwezi septemba mwaka 2005 wakati nilipokabidhiwa bendera ya kikosi cha uchukuzi na amiri jeshi mkuu wa sehemu ya jeshi letu, niliona hilo ni jambo takatifu, nilifurahi sana."

    Mwezi Mei mwaka 2006 Zhang Yong na kikosi chake cha uchukuzi walitumwa nchini Sudan kwenda kukaa huko kwa karibu mwaka mmoja. Mara baada ya kurudi nyumbani, alifunga safari na kuelekea tena Sudan kushiriki tena kwenye operesheni ya kulinda amani huko Waw kusini mwa Sudan mwezi Septemba mwaka 2007. Katika operesheni hiyo, kazi kuu ya kikosi cha China ilikuwa ni kujenga barabara, madaraja, vifaa vya kutoa maji na umeme, kusafirisha watu na miundo mbinu ya matibabu. Mwezi Aprili Mwaka 2008 wakati Zhang Yong na kikundi chake waliposafirisha vifaa vya shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF, walikutana na kundi la watu wenye silaha.


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako