• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bw. Zhang Yong, balozi wa Urafiki kati ya China na Sudan

    (GMT+08:00) 2009-11-20 18:52:41

    "Tuliona watu wengi wakitukimbilia kwa kasi kwa ghafla kutoka kwenye sehemu ya karibu. Kisha magari saba nane yaliyokuwa yamewabeba askari yalikwenda huko, na hali ilikuwa ya wasiwasi. Baada ya kuona hali hii nilijiambia tulia! Wanajeshi wengine wananitegemea! Niliwaza huku nikitoa amri ya kwamba, chukua tahadhari! Jifiche haraka! Wakati huo niliona kuwa dereva msaidizi Wu Zhicai akijisetiri vizuri nguo yake ya kujikinga dhidi ya risasi."

    Wakati huo naibu amiri jeshi Jenerali Mutsumi alimwambia Zhang Yong kwamba kutokana na hatari kubwa iliyowakabili, ni bora wapige kambi huko huko, na kuendelea na safari siku inayofuata. Lakini Zhang Yong aliamua kuendelea na safari yake mara moja kwa kufuata njia nyingine. Walipita kwenye vituo 17 vya ukaguzi njiani, kila mara Zhang Yong alishuka kutoka kwenye gari na kuwasiliana na wanajeshi waliokuwa kwenye vituo hivyo bila kujali hatari iliyokuwepo, sababu anajua kwamba kikosi chake kilikuwa kinasafirisha mahema kwa ajili ya watoto wanaosoma shuleni, bila mahema wasingeweza kuendelea na masomo yao katika majira ya mvua. Zhang Yong akikumbusha alisema:

    "Niliyofikiria ni kuhifadhi yale mahema 60, yakilinganishwa na mahema hayo, mambo mengine hayakuwa muhimu."

    Zhang Yong akiwa ofisa wa jeshi la kulinda amani, mbali na kumaliza kazi yake ya ulinzi wa amani, pia aliongoza wanajeshi wengine kushiriki kwenye shughuli za kutoa misaada ya kibinadamu, kama vile kutoa vifaa vya utoaji wa maji kwa ajili ya kituo cha maji kwenye sehemu ya Waw, kuboresha zana na vifaa vya matibabu vya hospitali ya Waw, kutoa mafunzo kwa madaktari, kutoa misaada ya kiufundi katika hospitali hiyo, na kutoa matibabu bila malipo kwa wenyeji vipofu karibu mia moja, na kuwarudishia uwezo wao wa kuona.


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako