• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bw. Zhang Yong, balozi wa Urafiki kati ya China na Sudan

    (GMT+08:00) 2009-11-20 18:52:41

    Kutokana na vitendo vyao kama hivyo, wanajeshi wa kulinda amani wa China wanaheshimiwa na kusifiwa na wanajeshi wa nchi nyingine, serikali ya Sudan na vyombo vya habari vya nchi mbalimbali. Amiri jeshi mkuu wa jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa nchini Sudan Bw. Fred Babi alimwita Zhang Yong kuwa ni "balozi wa urafiki kati ya China na Sudan". Akisema:

    "Nilifanya kazi pamoja naye kwa miaka mitatu, picha kubwa aliyonipa ni kwamba akiwa kamanda mwandamizi wa jeshi, yeye mwenyewe alishiriki kwenye kazi za kujenga ukuta, barabara, madaraja katika sehemu zilizokumbwa na vita, yeye mwenyewe alishiriki kwenye kufagia shule na hospitali, kutoa maelekezo ya matibabu kwa madaktari wa huko na kutoa dawa mbalimbali, ni vigumu kwangu kuamini kama hivyo ni vitendo vya kamanda mwandamizi. Niliwahi kuwa na ushirikiano na vikosi vya kulinda amani vya nchi mbalimbali, kikosi cha China kiliwajibika kuisaidia Afrika kukabiliana na changamoto zinazoikabili, na vitendo vyao vimewapa wananchi na maofisa wa serikali ya Sudan picha nzuri. "

    Kati ya mwaka 2005 na mwaka 2008, Zhang Yong alitumia wakati wake wote kwenye kazi ya ulinzi wa amani nchini Sudan, hii sio rahisi kwa mtu mwenye umri wa zaidi ya miaka 50 kama Zhang Yong. Alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari hivi karibuni alisema, kama kutakuwa na fursa anapenda kwenda tena Afrika kutoa mchango wake kuwasaidia watu wa Afrika na kuimarisha urafiki kati ya China na Afrika.


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako