• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya mkoa wa Macau yaonesha sura ya utalii kwa njia mbalimbali

    (GMT+08:00) 2009-11-23 17:09:08

    Mkurugenzi wa idara ya utalii ya Macau Bw An Dongliang alisema mara kwa mara kuwa, idara ya utalii ya Macau imeweka lengo la kuvutia watalii kwa njia mbalimbali na kuendeleza shughuli za utalii za aina mbalimbali. Macau pia inahimiza maendeleo ya shughuli za utalii zinazoonesha utamaduni kwa kutegemea vivutio vyake vya utalii; kubuni na kuendeleza shughuli za utalii zenye kauli-mbiu mbalimbali, ili kuongeza umaarufu wa utalii wa Macau.

    Kabla Macau kurejea nchini China, watalii wengi walikuwa wanatoka Hong Kong. Idadi ya jumla ya watalii walioitembelea Macau mwaka 1999 ni zaidi ya milioni 7.44. Mwezi Julai mwaka 2003 China bara ilianzisha "matembezi ya huria" katika mikoa ya Hong Kong na Macau kwa wakazi wake, ambapo kulikuwa na mabadiliko katika muundo wa watalii, na idadi ya watalii kutoka China bara iliongezeka mwaka hadi mwaka. Katika miaka ya hivi karibuni, idadi ya watalii kutoka China bara walioshiriki kwenye "matembezi ya huria" ya kuitembelea Macau ilichukua nusu ya idadi ya watalii walioitembelea Macau. Idadi ya watalii kutoka nchini na nchi za nje ilifikia kiasi cha milioni 22.9 mwaka 2008, ikiwa ni maradufu kuliko ile ya kabla ya Macau kurejea China. Hivi sasa ingawa hali ya shughuli za utalii si nzuri sana, lakini Macau inaanza kurejea katika hali ile nzuri ya zamani, mkurugenzi wa idara ya utalii ya Macau Bw An Dongliang alisema

    "Dalili nzuri inaonekana hatua kwa hatua katika shughuli za utalii za Macau, hivi sasa Macau inaendelea kuondokana na athari zilizosababishwa na msukosuko wa fedha duniani na homa ya mafua ya H1N1 aina ya A. Idadi ya watalii wanaotembelea Macau iliongezeka kwa mfululizo katika miezi mitatu iliyopita ikiwa ni ongezeko la 6.41% katika mwezi Agosti, 3.75% mwezi Septemba na 5.19% mwezi Oktoba ikilinganishwa na zile za mwaka uliopita katika vipindi kama hivi. Tukijumuisha hali hii pamoja na takwimu nyingine za kiuchumi, tunatarajia kuwa shughuli za utalii zinaendelea kuelekea kufufuka zaidi".


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako