Katika miaka ya hivi karibuni, idara ya utalii ya serikali ya Macau, shughuli za utalii na mashirika ya ndege ya huko zilitoa kwa pamoja "safari ya utalii kwenye sehemu zenye mabaki ya utamaduni", na kuwafahamisha watalii wa kutoka nchini na nchi za nje kuhusu Macau yenye vivutio na mambo mengi ya kufurahisha. Macau imekuwa na historia ya maingiliano ya utamaduni wa China na nchi za magharibi ya zaidi ya miaka 400, kwenye sehemu ya mji kuna nyumba za zamani zenye mitindo ya jadi ya kichina, mahekalu ya enzi za Ming na Qing, vilevile kuna majengo ya mtindo wa Ulaya ya kusini na makanisa yenye mtindo wa Baroque, vilevile kuna majengo ya kisasa, na yote hayo yanawapa watalii kumbukumbu nyingi. Bw Liu amefanya kazi huko Macau kwa miaka zaidi ya minne, alipozungumzia kumbukumbu yake kuhusu Macau alisema:
"Nimeishi Macau kwa zaidi ya miaka minne, zamani sikuwa na kumbukumbu nyingi kuhusu Macau, isipokuwa nilifahamu kuwa Macau kuna michezo ya kamari, lango kubwa la mawe la Sanba na hekalu la Mage. Baada ya kufika Macau nikafahamu kuwa mji huu mdogo wenye mchanganyiko wa utamaduni wa China na nchi za magharibi kuna mambo mengi, ambayo watu wa sehemu nyingine hawayafahamu. Kwa mfano, sehemu nyingi za mjini zenye mabaki ya utamaduni zikiwa ni pamoja na Longhuanpuyun, ukumbi wa waridi, jumba la michezo la Gangding, ofisi kuu ya posta na klabu ya jeshi la nchi kavu ambazo watu wengi hawazifahamu. Kila mwaka sherehe nyingi zinafanyika Macau, mbali na sikukuu za jadi za Spring, kupiga makasia kwenye mashua za dragon, wakazi wa Macau vilevile wanasherehekea sikukuu ya krismas, siku ya wapendanao, siku ya mama mtakatifu na siku ya kuwaombea marehemu, kwa hiyo tunasema wakazi wa Makau wamebahatika. Chakula cha Macau pia kina umaalum wake, mbali na vyakula vya jadi vikwemo soseji ya nyama ya nguruwe yenye umaalumu wa mkoa wa Guangdong, maandazi ya kichina yenye nyama ya nguruwe ndani yake(bao zi), uji uliopikwa pamoja na nyama na mayai ya bata yaliyotengenezwa kwa njia maalumu, vilevile kuna keki yenye mayai ya mtindo wa Ureno na keki zenye vipande vya mbegu ya apricot, ambazo zimechanganywa kwa umaalum wa kireno, hivyo wakazi wa Macau pamoja na watalii wanaotembelea huko wana bahati nzuri ya kuonja vyakula vingi maarufu."
Katika miaka zaidi ya kumi tangu Macau irejee China, serikali ya huko licha ya kuendeleza, kuhifadhi na kuonesha rasilimali zilizopo sasa, kila mwaka inafanya shughuli za aina mbalimbali za michezo ya kimataifa, ambazo zimechangia kufahamika zaidi kwa jina la Macau. Mtalii mmoja kutoka mkoa wa Shandong alisema, "Ninaona Macau ni nzuri, kila kitu cha hapa ni kizuri, baada ya mimi kurejea nyumbani, nitawafahamisha marafiki zangu."
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |