• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya mkoa wa Macau yaonesha sura ya utalii kwa njia mbalimbali

    (GMT+08:00) 2009-11-23 17:09:08

    Mapema mwaka 2002, serikali ya mkoa wa utawala maalumu wa Macau ilianza kutoa ombi kwa shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO kuiorodhesha "sehemu ya mji ya Macau" kuwa mabaki ya utamaduni ya dunia. Baada ya kufanya jitihada kwa miaka mitatu, tarehe 15 Julai mwaka 2005 mkutano wa 29 wa kamati ya urithi ya dunia uliamua kuiorodhesha "sehemu ya mji ya kihistoria ya Macau" kuwa urithi wa utamaduni wa dunia. Tokea hapo kundi hili la majengo yanayoonesha historia ya maingiliano ya utamaduni kati ya China na nchi za magharibi limekuwa urithi wa 31 wa utamaduni wa dunia.

    "Sehemu ya mji ya kihistoria ya Macau" ni sehemu ya majengo yenye mitindo ya ujenzi ya China na ya nchi za magharibi, ambayo ina majengo mengi ya zamani sana, na kuhifadhiwa vizuri hadi hivi sasa nchini China, kati ya hayo majengo zaidi ya 20 ni ya kale.

    Mwaka 2006, Macau ikishirikiana na mkoa wa Guangdong na Hong Kong ilitoa ombi la kwanza la kuweka "opera ya Yue" na "chai ya baridi" katika "orodha ya mabaki ya utamaduni wa vitu visivyoonekana vya ngazi ya taifa". Mwezi Juni mwaka 2008, "uchongaji wa mbao--kinyago cha mungu wa Macau" uliorodheshwa kwenye mkupuo wa pili wa orodha ya urithi wa utamaduni, na kuwa urithi wa kwanza wa utamaduni wa vitu visivyoonekana vya ngazi ya taifa uliotolewa na Macau peke yake. Habari zinasema, keki ya mayai yenye umaalumu wa kireno na ngoma ya Tufeng vimewekwa katika mchakato wa kutoa ombi la kuorodheshwa kuwa urithi wa utamaduni wa vitu visivyoonekana vya Macau. Sura ya asili ya duka la rehani ya zamani "Dechengan" itaoneshwa kwenye maonesho ya kimataifa ya Shanghai mwaka 2010, ili watu waone ufanisi wa Macao katika kukarabati na kutumia majengo ya kihistoria.


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako