• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tarafa ya kale Heshun yenye mvuto

    (GMT+08:00) 2009-11-30 16:47:56

    Kwenye sehemu ya mpaka kati ya mkoa wa Yunnan, China na Myanmar kuna tarafa moja inayoitwa Heshun, ambayo ina historia ya miaka 600. Tarafa ya Heshun iko kwenye wilaya ya Tengchong mkoani Yunnan. Kama ukisafiri kwenye barabara safi na nzuri kutoka mji mkuu wa wilaya kuelekea upande wa kusini magharibi, na kupita kwenye mashamba ya mpunga na mito, nyumba za wakazi zikaonekana kwenye mtelemko wa mlima. Hii ndio tarafa ya Heshun.

    Mara tu baada ya kuingia kwenye tarafa ya Heshun, watu wanaona hali ya ushwari na neema ya sehemu za mashambani. Ndani ya tarafa hiyo ya kale, vichochoro vinaunganisha pamoja nyumba za zamani zenye kuta za rangi nyeupe na mapaa yenye vigae vya rangi ya kijivu iliyokolea, ukumbi mkubwa nadhifu wa jadi wa kuwekea vibao vya mizimu ya mababu wa kale, na mabanda yaliyotengenezwa maridadi sana, katika tarafa hiyo kuna miti mingi ya kale, ambapo wakazi wanapumzika au kuzungumza wakiwa wameketi kwenye vigoda vya mawe vilivyoko kivulini. Nje ya tarafa kuna mashamba mengi ya mpunga, ambapo ndege weupe aina ya Egret wakiruka na kutua mara kwa mara; ndani ya mabwawa kuna maji mengi na maua ya yungiyungi, kuna wazee wanaovua samaki kwa ndoano, mandhari hii ya mashambani ni ya kuvutia sana!


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako