Mkazi wa tarafa hiyo Bw Liu Fuqing alisema, maktaba ni mahali muhimu ambapo yeye anakwenda kusoma, kila siku baada ya kutoka kazini huwa anafika katika maktaba kusoma magazeti na data anazozihitaji. Anasema lengo la kujenga maktaba hii ni muhimu sana na ina manufaa ya muda mrefu kwa wakazi wa huko. Alisema,
"Umetolewa wito wa kujenga jamii yenye masikilizano, ulitolewa hivi sasa, lakini wakazi wa tarafa yetu hii walitoa wito wa kujenga tarafa yenye amani na masikilizano miaka mia kadhaa iliyopita wakati walipojenga lango la kumbukumbu la mawe, hii inaonesha kuwa watu wanatarajia sana jamii yenye mapatano na masikilizano kati ya maumbile, ardhi na watu. Tarafa ya Heshun ni sehemu inayotilia maanani sana mambo yanayohusu maadili. Sifa za wakazi wa Heshun zinatokana na mchango unaotokana na maktaba ya Heshun. Katika tarafa ya Heshun utaona wakazi wake ni wapole na wanaofuata sana maadili."
Mazingira bora ya kimaumbile, mienendo mizuri ya wakazi na msingi mkubwa wa utamaduni, yote hayo yanawavutia sana watalii. Mtalii kutoka mkoa wa Sichuan Bw Zhang alisema, ingawa katika miaka ya hivi karibuni sehemu ya utalii ya Heshun imeendelezwa zaidi, lakini sehemu hiyo yenye msingi mkubwa wa utamaduni wa huko inastahili kutembelewa na watu. Alisema,
"Tarafa hii ina vitabu karibu elfu 80, si jambo la kawaida, tena vitabu vyake ni vya kutoka zamani sana vya wakati wa kupambana na mashambulizi dhidi ya uvamizi wa Japan."
Heshun ni tarafa ya kale, hadi hivi sasa wakazi wa huko bado wanaishi katika nyumba za zamani zilizojengwa kwa matofali na mbao. Kuendelezwa kwa shughuli za utalii kwenye tarafa ya Heshun kumeleta mabadiliko kwenye maisha ya wakazi wa huko kutokana na ongezeko la idadi ya watalii. Mbunge wa tarafa ya Heshun, ambaye ni msimamizi wa shughuli za utalii za huko Bw Yin Shaopo alisema, wakazi wa Heshun ni wachangamfu na wanapenda kufungua mlango kwa nje, kufika huko kwa watalii wengi kunaleta utamaduni na mawazo ya kisasa, hili ni jambo zuri.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |