• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tarafa ya kale Heshun yenye mvuto

    (GMT+08:00) 2009-11-30 16:47:56

    Katika tarafa ya Heshun kuna mabanda ya kufulia nguo, ambayo ni majengo maalumu yanayohusiana na maisha ya watu. Tukitaka kueleza kuhusu mabanda ya kufulia nguo hatuna budi kuyaeleza kuanzia tarafa ya Heshun, ambayo ni maskani ya wachina wanaoishi katika nchi za nje toka miaka mingi iliyopita. Tarafa ya Heshun iko kwenye sehemu inayopakana na nchi ya Myanmar. Katika zamani za kale, Asia ya kusini na Asia ya kusini mashariki ziliitwa na wakazi wa tarafa ya Heshun kuwa ni "sehemu za Yi", yaani sehemu ya watu wa mashariki, kwa kawaida wanaume wote walikuwa wanakwenda "sehemu za Yi" kufanya shughuli za biashara na kujenga msingi wa maisha. Wanaume walioondoka kwao waliwakumbuka sana watu wa familia zao, ili kuwawezesha wanawake waliobaki kwao wapate mahali pa kujisetiri wakati upepo mkali ukivuma na mvua ikinyesha wanapoenda kufua nguo kwenye mabwawa, watu hao walitoa mchango wa fedha toka katika utawala wa Guangxu wa enzi ya Qing, hatimaye yalijengwa mabanda mengi ya aina mbalimbali ya kufulia nguo.

    Hadi sasa ni miaka mingi imepita, ingawa watu waliojenga mabanda hayo hawapo, lakini sauti ya kufua nguo bado inasikika kwenye mabanda hayo. Kwenye tarafa hiyo hakuna kelele kama zile katika miji mikubwa, watu wa sehemu hii wanaendelea kudumisha mtindo wa maisha yao ya jadi, wanawake wanapenda kuitana kwenda kufua nguo pamoja kwenye mabanda hayo. Mkazi wa tarafa hii Zhao Xiuxing alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, ingawa familia yake imeshanunua mashine ya kufulia nguo, lakini anaendelea kupenda kufua nguo kwenye mabanda hayo. Alisema

    "Kila siku ninakwenda kufua nguo kwenye mabanda hayo, kwa mfano ninapofua mashuka ninapenda kuyafua kwenye mabanda yale, tuna mashine ya kufulia nguo nyumbani kwangu, lakini sipendi kuitumia, tena inatumia umeme na sabuni nyingi ya unga, nikienda kufua kwenye mabanda tunaweza kufua nguo huku tukipiga soga. Mabanda ya kufulia nguo ni mahali pazuri pa kupiga soga, vilevile ni mahali pazuri pa kufanya maingiliano na watu."

    Mtu akitembea kwenye tarafa ya Heshun, mara kwa mara anaweza kuona vitu vya kihistoria na kiutamaduni. Wakazi wa Heshun wameunganisha vizuri shughuli za kilimo, kibiashara na kuheshimu mawazo ya Confucius. Wanajiendeleza kielimu na kiutamaduni kizazi hadi kizazi. Huko pia kuna maktaba ya Heshun, ambayo ilianzishwa mapema na ni kubwa zaidi kwenye sehemu ya vijijini ya China. Maktaba hii sasa ina vitabu karibu elfu 80, na vingi ni vitabu adimu sana nchini China. Mfanyakazi wa maktaba alisema, hivi sasa idadi ya wakazi wa tarafa ya Heshun ni zaidi ya 6,000, na watu zaidi ya 3,000 wamepata kadi za kuazima vitabu. Mkuu wa maktaba ya tarafa ya Heshun Bw Cun Maohong alipozungumzia historia ya kuanzishwa kwa maktaba hiyo alisema, wakazi wa tarafa ya Heshun wana jadi ya kutilia mkazo katika mambo ya utamaduni na elimu. Alisema

    "Katika muda mrefu wa miaka mia kadhaa iliyopita, mababu zetu wa kale walifahamu ukweli mmoja kuwa tukitaka maskani yetu iondokane na hali ya unyonge na kupata maendeleo, hatuna budi kuendeleza mambo ya utamaduni na elimu, kutokana na wazo hilo maktaba ya Heshun ilijengwa mwaka 1928 na shule ya kati Yiqun ilijengwa mwaka 1940."


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako