• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vyakula maalumu vya Boao

    (GMT+08:00) 2009-12-07 17:07:16

    Kwenye mji wa Qionghai wa kisiwa cha Hainan, kusini mwa China kuna tarafa moja ndogo iitwayo Boao, ambayo sasa imekuwa maarufu sana kutokana na kuchaguliwa kuwa mahali pa kudumu pa kufanya mikutano ya "Baraza la Asia". Sehemu hii licha ya kuwa na mandhari nzuri ya anga ya buluu na pwani yenye minazi, kuna chakula maalumu cha kuvutia.

    Boao inasifiwa kama "tarafa ya peponi", ni rahisi kwa watu kupata chakula maalumu cha huko katika vibanda vya chakula cha baharini vilivyoko kwenye sehemu ya kati ya tarafa hii. Mwongoza watalii kijana Zhang alitushauri kwanza tuonje supu moja iitwayo supu ya punje za unga wa mchele na mhenzirani wa kinyesi cha kuku. Kijana Zhang alisema, jina la supu hiyo si zuri, lakini supu hiyo haipatikani katika sehemu yoyote nyingine isipokuwa huko tu. Alisema"Mhenzirani wa kinyesi cha kuku ni aina ya mmea unaopandwa kwenye mlima karibu na mto Wanquan. Baada ya mhenzirani kupondwa na kusagwa pamoja na mchele kuwa unga ambao unatengenezwa kuwa punje, punje zinachemshwa katika maji na kuwekwa sukari, na maziwa yenye juisi ya nazi."

    Kijana Zhang alisema, supu hii licha ya kuwa na ladha nzuri, pia inajenga mwili. Wakazi wa huko wanakunywa supu hiyo katika miezi ya Julai na Agosti.

    Mbali na supu hiyo, kitoweo cha kuku aliyepikwa kwa tui la nazi, ni moja kati ya vitoweo maarufu katika kisiwa cha Hainan, ambacho kwa tarafa ya Boao ni kitoweo chenye umaalumu zaidi. Kijana Zhang alisema, kitoweo hiki kina historia ya miongo kadhaa katika tarafa ya Boao, ambacho kilivumbuliwa na mpishi mmoja wa hoteli maarufu ya Qiongnan ya mji wa Haikou, mpishi huyu alianza kuitwa "baba wa nne wa Qiongnan" kutokana na kitoweo hicho kizuri. Hivi sasa tawi la hoteli hiyo limeanzishwa katika tarafa ya Boao. Kijana Zhang alisema, kuku wanaotumiwa katika kupika kitoweo kicho ni sharti wawe ni kuku Wenchang wanaofugwa na wakazi wa huko, kuku wa aina hii wanakula mbegu za aina miti wa banyan, ladha ya kitoweo cha kuku ni nzuri sana na ni tofauti na vitoweo vya kuku vya sehemu nyingine kutokana na kuku kupikwa kwa kutiwa tui la nazi. Alisema

    "Kuku Wenchang, kutiwa supu, vipande vya tangawizi, vitungu vya kijani, na pombe ya Shaoxing, kisha anachemshwa kwa mvuke kwa nusu saa, baada ya kutolewa, anatiwa maziwa, tui la nazi, kiungo cha kuongeza ladha ya chakula na sukari, kisha anakaangwa kwa moto mkubwa na kuongeza kidogo rojo ya unga wa mahindi. Kitoweo hiki ni kitamu na kina harufu nzuri ya nazi".


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako