• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vyakula maalumu vya Boao

    (GMT+08:00) 2009-12-07 17:07:16

    Mbali na kitoweo hiki maarufu, kuna wali yenye gimbi, ambayo ni chakula cha jadi katika kisiwa cha Hainan, na vilevile kinapatikana katika tarafa ya Boao. Mwongoza watalii kijana Zhang alisema,

    "Vitu muhimu vya chakula hicho ni mchele na jimbi, kinatiwa kidogo vipande vidogo vya nazi, vitunguu saumu vilivyopondwa na vipande vidogo vya tangawizi. Wali hii ni laini na yenye ladha ya nazi."

    Kwa kuwa Boao iko karibu na bahari, hivyo ina mazao mengi maalumu ya baharini. Upande wa kusini kabisa wa Boao ni mahali ambapo maji ya mto Wanquan yanaingia baharini, huko kuna ufukwe wenye mchanga mweupe kabisa ulio na urefu wa kilomita 8.5, huko ni mahali ambapo watalii hawakosi kufika. Ufukwe huu unatenganisha maji ya mto na maji ya bahari. Mtu akisimama huko, mbele yake ni bahari yenye mawimbi makubwa, lakini nyuma yake ni maji shwari ya mto. Kwenye ufukwe huu kuna mkahawa mmoja, mwenye mkahawa alitushauri tule vitoweo vya samaki wa aina mbalimbali, ambavyo ni maarufu kwenye mkahawa huo. Alisema"Samaki wa hapa ni wazuri sana, kwa kuwa samaki wanaoishi hapa penye makutano ya maji ya mto na bahari, hivyo maji ya hapa hayana chumvi nyingi, ndio maana samaki wa hapa ni laini na wenye ladha nzuri. Hapa kuna aina nyingi za samaki, kuna kiasi cha aina 600. Ngozi za samaki wa hapa ni kama zenye mwangaza, na nyama yake ni nyeupe pee, hawapatikani katika sehemu nyingine."

    Samaki aliyetushauri sana mwenye mkahawa ni samaki anayeitwa Dongxingban, sehemu nzuri zaidi ya samaki huyu ni kichwa na mkia wake. Hii ni kwa sababu gani? Mwenye mkahawa alisema

    "Kichwa na mkia wake ni vitamu zaidi, kichwa na mkia wake vina mafuta mengi, samaki anapoogelea katika maji, mkia wake unafanya kazi zaidi, hivyo nyama yake ni tamu zaidi, sehemu ya tumbo ni laini, kwa hiyo sehemu hizo ni bora zaidi."


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako