• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ndoa kati ya wachina na waafrika imekuwa ni sehemu ya kubadilishana utamaduni

    (GMT+08:00) 2014-11-13 14:16:12

    Yue Yujiao kutoka China na Olusegun Adekanmi wakieleza vile walivyopatana.

    Adekanmi alikuja china miaka 6 iliopita na amekuwa akimchumbia Yujiao kwa miaka mitatu kabla ya kuamua kufunga ndoa naye.anasema hakujali tamaduni za kichina na hakutaka ziwe kikwazo cha mapenzi yake kwa Yue Yujiao.

    Mwanamme wa kifarika na bibi yake Mchina pia walihudhuria harusi ya Yue Yujiao na Olusegun Adekanmi kwenye ubalozi wa Nigeria mjini Beijing China. Idadi ya waafrika wanaofunga ndoa na wachina imeendelea kuongezeka.

    Yue Yujiao na Olusegun Adekanmi wapigana busu baada ya kutangazwa kuwa bibi na bwana. Mwanzoni, Yue Yujiao alikuwa na uoga kiasi wa kuwa na mchumba wa kiafrika lakini baada ya kukolea kwenye mapenzi ya Adekanmi yuko tayari kuandamana na mume wake hadi nchini Nigeria.

    Picha ya pamoja na baadhi ya wageni wachina na waafrika waliohudhuria harusi ya Yue Yujiao na Olusegun Adekanmi.

    Picha ya harusi ya Shui Li Fang na bwana yake Ole Chuku ambao walioana miaka 16 iliyopita na wamejaliwa watoto watatu. Taakwimu zinaonyesha kwamba kuna kati ya wanaume 50 na 60 wa Nigeria ambao wameoa wachina. Li Fang anasema haoni tofauti kuolewa na mwanaume kutoka sehemu yoyote duniani muhimu kwake ni mapenzi, kuelewana na kulea familia

    Familia ya Shui Li Fang na bwana yake Ole Chuku. Huku biashara kati ya Afrika na china ikiongezeka kwa zaidi ya dola bilioni 200 za kimarekani, pia uhusiano wa watu kwa watu unapiga hatua kupitia kwa ndoa kama hizi.


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako