• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 29-Novemba 4)

    (GMT+08:00) 2016-11-04 17:18:03

    China yarusha angani roketi kubwa zaidi kuwahi kuundwa

    Uchina imerusha angani roketi kubwa zaidi kuwahi kuundwa katika taifa hilo, roketi iliyopewa jina Long March 5.

    Roketi hiyo ilirushwa angani kutoka kituo cha shughuli za anga za juu cha Wenchang katika mkoa wa Hainan.

    Imebeba setilaiti ya kufanya majaribio ambayo imepewa jina Shijian-17.

    Long March 5 inaipa Uchina uwezo wa kupeleka angani mitambo na mizigo mizito, kwa mfano mitambo ya kutumiwa kwa ajili ya mawasiliano na vifaa vya kuunda kituo cha anga za juu ambacho taifa hilo linapanga kujenga katika anga za juu.

    Maelezo ya roketi hiyo yanaashiria ina uwezo wa kubeba tani 25 hadi mzingo wa chini wa dunia (LEO), kilomita kadha juu angani, na tani 14 hadi mzingo wa mbali wa dunia, ambao ni kilomita 36,000 kutoka ardhini.

    Long March 5 imo kwenye kitengo sawa na cha roketi yenye nguvu zaidi ya Marekani, roketi ya Delta-IV Heavy.

    Kampuni za Marekani za SpaceX na Blue Origin zinaunda vyombo vya anga za juu vyenye uwezo wa kusafirisha tani zaidi ya 50 katika mzingo wa chini wa dunia (LEO).

    1 2 3 4 5 6 7 8
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako