• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Disemba 17-23)

  (GMT+08:00) 2016-12-23 20:56:51

  Umoja wa Mataifa wahimiza DRC kupunguza hali ya wasiwasi kuhusu uchaguzi

  Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw Ban Ki-moon amewahimiza viongozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wapunguze hali ya wasiwasi ili kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya ya uchaguzi.

  Rais Joseph Kabila wa nchi hiyo amemaliza muda wa kuwa madarakani tarehe 19 mwezi huu, lakini uchaguzi wa urais haujafanyika kwa wakati, hali ambayo imesababisha malalamiko ya wananchi.

  Taarifa iliyotolewa na Bw Ban Ki-moon imelaani makabiliano yaliyosababisha vifo na majeruhi kati ya vikosi vya usalama na wapinzani. Amesisitiza kuwa vikosi vya usalama vinatakiwa kuwa na uhimili katika kulinda utaratibu wa umma. Pia ametoa wito kwa pande zote za kisiasa zijizuie .


  1 2 3 4 5 6 7 8
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako