• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Disemba 17-23)

  (GMT+08:00) 2016-12-23 20:56:51

  Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika atoa wito wa kushirikiana kujenga Afrika yenye ustawi zaidi

  Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Nkosazana Dlamini-Zuma ametoa wito kwa watu wa Afrika kufanya juhudi kwa pamoja ili kujenga Afrika yenye ustawi zaidi kwa vijazi vijavyo.

  Akizungumzia hali ya Umoja huo mjini Durban, Afrika Kusini, Bibi Zuma amesema nchi za Afrika zitatekeleza kithabiti mpango wa Ajenda ya Maendeleo ya Mwaka 2063. Amesema serikali za nchi mbalimbali za Afrika zimefikia maoni ya pamoja kuhusu kuufadhili Umoja wa Afrika kwa kutoa asilimia 0.2 ya pato la ushuru, hivyo kukusanya dola za kimarekani bilioni 1.2 kwa Umoja huo kila mwaka, ambayo ni sawa na asilimia 76 ya thamani ya misaada kutoka nje iliyopo sasa.

  Bibi Dlamini Zuma ameongeza kuwa, nchi za Afrika zinapaswa kuharakisha mchakato wa utandawazi kwa kupitia kujenga soko la pamoja, miundombinu na kuhimiza uhamaji wa watu, ili kuleta maendeleo ya pamoja.


  1 2 3 4 5 6 7 8
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako