• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 28-Februari 3)

    (GMT+08:00) 2017-02-03 17:48:15

    Waliofurushwa na Trump Marekani wakwama Ethiopia

    Zaidi ya watu 100 wamekwama katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole mjini Addis Ababa nchini Ethiopia baada ya kufurushwa nchini Marekani kulingana na waziri wa habari nchini humo.

    Hatua hiyo inafuatia agizo la rais Donald Trump kusitisha mpango wa wakimbizi kuingia nchini humo mbali na kuzuia kuingia kwa raia wa mataifa saba ya Kiislamu ikiwemo Yemen, Libya,Sudan na Somalia.

    Awali msemaji wa serikali ya Kenya Bw. Eric Kiraithe alitangaza pia kwamba zaidi ya raia 90 wa Somalia na Kenya wamewasili Nairobi baada ya kufukuzwa Marekani.

    Bw. Kiraithe amesema waliofukuzwa ni wanaume 90 kutoka Somalia na wanawake wawili kutoka Kenya, lakini amesema hajui ni kwa nini wamefukuzwa kutoka Marekani.


    1 2 3 4 5 6 7 8
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako