• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 28-Februari 3)

    (GMT+08:00) 2017-02-03 17:48:15

    Rais wa Tanzania amteua mkuu mpya wa jeshi

    Rais John Pombe Magufuli amemteua Luteni Jenerali Venance Mabeyo kuwa mkuu wa majeshi ya Ulinzi nchini Tanzania akichukua mahala pake jenerali Davis Mwamunyange aliyestaafu.

    Taarifa kutoka ikulu iliotumwa katika vyombo vya habari inasema kuwa Luteni huyo sasa amepandishwa cheo na kuwa jenerali kamili.

    Wakati huohuo rais amemteua meja jenerali James Mwakibolwa kuwa mnadhimu mkuu wa majeshi ya ulinzi akichukua mahala pake Jenerali Mabeyo.Pia yeye alipandishwa cheo cha luteni jenerali.

    Rais amesema kuwa uteuzi huo unaanza kutekelezwa mara moja.

    Tarehe ya kuapishwa kwa wawili hao itatangazwa baadaye.


    1 2 3 4 5 6 7 8
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako