• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Februari 4-Februari 10)

    (GMT+08:00) 2017-02-10 17:42:49

    Jumuiya ya kimataifa yailaani Israel kwa kuhalalisha maeneo ya makazi Ukingo wa Magharibi

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw Antonio Guterres ametoa taarifa ikisema sheria ya Israel ya kuhalalisha maeneo ya makazi yaliyoko Ukingo wa Magharibi inakiuka sheria ya kimataifa.

    Taarifa hiyo imesema hatua hiyo ya Israel itakuwa na athari kubwa ya kisheria kwa Israel. Bw Guterres amesisitiza kwamba masuala yote makuu yanatakiwa kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo ya moja kwa moja kwenye msingi wa maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na makubaliano ya pamoja.

    Ofisa wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia sera za kidiplomasia na usalama Bibi Federica Mogherini amelaani sheria hiyo ya Israel akionya kwamba sheria hiyo "imevuka mstari mwekundu".

    Rais Mahmoud Abbas wa Palestina amesema sheria hiyo ya Israel "inakanyaga sheria za kimataifa". Ametoa wito wa kuhimiza utekelezaji wa azimio namba 2334 lililopitishwa mwishoni mwa mwaka jana na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.


    1 2 3 4 5 6 7
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako