• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Februari 4-Februari 10)

    (GMT+08:00) 2017-02-10 17:42:49

    Rais wa Syria awapokea mateka wanawake na watoto walioachiwa huru na waasi

    Rais Bashar al-Assad wa Syria na mke wake Bibi Asma Assad, wamewapokea mateka wanawake na watoto walioachiwa huru hivi karibuni na makundi ya waasi.

    Wanawake na watoto hao walitekwa nyara miaka mitatu na nusu iliyopita katika mkoa wa Latakia kusini magharibi mwa Syria, baada ya waasi kuvamia maeneo ya pembezoni mwa mkoa huo. Waliachiwa huru jumatano wiki hii wakati wa mabadilishano kati ya serikali na waasi.

    Wanawake 54 na watoto wao walijumuishwa kwenye mabadilishano hayo, ambapo serikali iliwaachia idadi kama hiyo ya waasi wanaoshikiliwa kwenye magereza ya serikali.

    Mabadilishano hayo yalifanyika kwenye eneo la pembezoni mwa mkoa wa Hama.


    1 2 3 4 5 6 7
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako