• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Februari 18-Februari 24)

    (GMT+08:00) 2017-02-24 18:08:26

    Eneo la Ziwa Tanganyika lakumbwa na tetemeko la ukubwa wa 5.7

    Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 5.7 kwenye vipimo vya Richter limekumba maeneo ya Ziwa Tanganyika usiku wa kuamkia Ijumaa na kutikisa maeneo ya kaskazini mwa Zambia na na pia kusikika maeneo ya kusini magharibi mwa Tanzania, hasa eneo la Rukwa.

    Kitovu cha tetemeko hilo, kwa mujibu wa Shirika la Utafiti wa Jiolojia la Marekani, kilikuwa kilomita 10 chini ya ardhi umbali wa kilomita 45 mashariki mwa mji wa Kaputa nchini Zambia.

    Tetemeko la ardhi la ukubwa kama huo huchukuliwa kuwa la kadiri lakini wataalamu wanasema kutokana na hali kwamba kitovu chake chakikuwa chini sana ndani ya ardhi, huenda hilo lilisababisha mitikisiko kuwa mikubwa.

    Septemba mwaka 2016, tetemeko jingine la ardhi lililotokea eneo la Bukoba, mkoani Kagera kaskazini mwa Tanzania.

    Watu 16 walifariki na wengine 250 kujeruhiwa kutokana na tetemeko hilo. Mamia wengine walibaki bila makao.


    1 2 3 4 5 6 7 8
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako