• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Februari 18-Februari 24)

    (GMT+08:00) 2017-02-24 18:08:26

    Kambi mpya ya wakimbizi yafunguliwa Uganda

    Msemaji wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa mataifa UNHCR limefungua kambi moja mpya ya wakimbizi kaskazini mwa Uganda, inayotarajiwa kupokea wakimbizi zaidi ya laki moja kutoka Sudan Kusini.

    Hatua hiyo imekuja baada ya kujaa kwa kambi nyingine iliyofunguliwa Desemba mwaka jana.

    Kwa sasa Sudan Kusini ni nchi inayotoa wakimbizi wengi zaidi duniani baada ya Syria na Afghanistan. Uganda imeanza kuona ugumu wa kupokea wakimbizi na inahitaji msaada wa haraka wa jumuiya ya kimataifa ili iweze kupokea wakimbizi.

    Shirika la Mpango wa Chakula ya Dunia (WFP) limesema limelazimika kupunguza kwa zaidi ya nusu msaada wa chakula kwa wakimbizi nchini Uganda kutokana na ukosefu wa fedha.

    Mbali na kufungua kambi hiyo, habari nyingine zinasema Sudan imetangaza kutoa misaada ya kibinadamu kwa Sudan Kusini.


    1 2 3 4 5 6 7 8
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako