• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (4 Machi-10 Machi)

    (GMT+08:00) 2017-03-10 20:14:55

    Polisi Afrika Kusini wazima maandamano dhidi ya raia wa kigeni

    Alhamisi wiki hii polisi wa Afrika Kusini walifyatua hewani risasi za mpira kuwatawanya waandamanaji walioingia mitaani kwa kile walichosema hawataki raia wa kigeninchini mwao. Maandamano hayo yalifanyika katika mji wa Johannesburg.

    Watu watano wamejeruhiwa katika maandamano hayo yaliyofanyika katika eneo la Reiger Park, kitongoji cha mji mkuu wa Afrika Kusini..

    Kwa wiki kadhaa, mashambulizi dhidi ya raia kutoka katika Ukanda wa Jangwa la Sahara yameendelea kushuhudiwa Johannesburg.

    Maandamano ya Alhamisi wiki hii yalihusu mgao wa makazi ya jamii kwa raia wa kigeni.

    Waandamanaji, ambao walichoma matairi na kujaribu kuchoma nyumba ya mwanasiasa wa Afrika Kusini, wanalalamika kuhusu serikali kushindwa kutoa huduma za msingi kama maji na umeme.

    Mwezi uliopita, maduka kadhaa na nyumba zinazomilikiwa na wahamiaji Waafrika zilivamiwa karibu na mji wa Pretoria.


    1 2 3 4 5 6 7 8 9
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako