• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (4 Machi-10 Machi)

    (GMT+08:00) 2017-03-10 20:14:55

    Aliyekuwa jenerali wa jeshi Sudan Kusini amezindua kundi lake la waasi

    Aliyekuwa jenerali wa cheo cha juu jeshini nchini Sudan Kusini Thomas Cirillo Swaka amezindua kundi lake la waasi kwa jina National Salvation Front.

    Kwenye taarifa yake ya Jumatatu Swaka anasema kundi lake hilo la waasi litalenga kupinga utawala wa Rais Salva Kirr.

    Hajataja ukubwa wa kundi lake hilo ambalo litafanya kazi na lile la Riek Machar la Sudan People's Liberation Army-in-Opposition (SPLA-IO).

    Swaka alijiuzulu mwezi uliopita (Februari 2017) akiwa naibu jenerali wa jeshi la serikali anayeshughulikia ugawaji.

    Alijiuzulu akilalamika kwamba Rais Kirr anaigawanya nchi kwa misingi ya kikabila.


    1 2 3 4 5 6 7 8 9
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako