• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (11 Machi-17 Machi)

  (GMT+08:00) 2017-03-17 18:36:53

  Msemaji wa polisi Uganda Felix Kaweesi na walinzi wake wawili wauwawa

  Msemaji wa jeshi la polisi nchini Uganda Felix Kaweesi na walinzi wake wawili wameuwawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana walipokuwa wanaondoka nyumbani kwa msemaji huyo.

  Bw Kaweesi alikuwa ameteuliwa mwaka jana tu kwenye wadhifa huo na ameuwawa kwenye eneo la Kulambiro, Kisaasi kaskazini mashariki mwa mji mkuu Kampala.

  Taarifa zinasema alikuwa njiani kwenda kuwahutubia wanafunzi katika chuo kikuu cha Uganda Christian University alipokumbana na mauti yake. Wanafunzi walikuwa tayari wamekusanyika ukumbini katika chuo hicho.

  Miili ya watatu hao imepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Mulago.


  1 2 3 4 5 6 7 8
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako