• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (11 Machi-17 Machi)

    (GMT+08:00) 2017-03-17 18:36:53

    Maharamia Somalia waiachilia bila fidia meli ya Sri Lanka

    Maharamia nchini Somalia wameiachilia bila fidia meli ya Sri Lanka iliyokua ikibeba mafuta ambayo walikua wameishikilia tangu mwanzoni mwa wiki hii.

    Kwa mujibu wa Kikosi cha majini cha Ulaya kinachopambana na uharamia Wafanyakazi wa meli hiyo kwa jina "Aris 13", wako salama, kikosi hicho.

    "Aris 13" ilikua imebeba mafuta na gesi kutoka Djibouti kuelekea Mogadishu wakati ilishambuliwa Jumatatu na watu wenye silaha katika meli mbili.

    Kikosi cha majini cha Ulaya dhidi ya uharamia kilisema Jumanne wiki hii kwamba kiliwasiliana na nahodha wa meli hiyo, ambaye aliwaambia kuwa maharamia wanadai fidia.

    Siku ya Alhamisi, kikosi cha walinzi katika pwani ya Puntland kimewatishia maharamia kukabiliana na kama wakataa kuiachia meli hiyo na wafanyakazi wake.


    1 2 3 4 5 6 7 8
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako