• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (18 Machi-24 Machi)

    (GMT+08:00) 2017-03-24 18:08:57

    Watu watano wauwawa kwenye shambulizi nje ya Bunge mjini London Uingereza

    Watu watano wameuwawa wiki hii na wengine zaidi ya 40 kujeruhiwa kwenye shambulizi nje ya Bunge mjini London.

    Habari kutoka Uingereza zinasema, mshambuliaji mmoja aliendesha gari lake kugonga watu kwenye daraja la Westminster, na halafu kumshambulia polisi kwa kisu nje ya bunge la nchi hiyo, kabla ya kuuawa kwa kupigwa risasi na polisi.

    Wakati shambulizi hilo likitokea waziri mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May alikuwa akijibu maswali ya wabunge ndani ya jengo la bunge.

    Mtu ambaye polisi wanaamini alihusika na shambulio hilo katika eneo la Westminister ametambuliwa rasmi kuwa Khalid Masood, kulingana na wapelelezi wa Scotland Yard.

    Masood mwenye umri wa miaka 52 alizaliwa katika eneo la Kent na wapelelezi wanaamini kwamba alikuwa akiishi Midlands magharibi.

    Masood hakuhusishwa katika uchunguzi wowote na hakuna ripoti yoyote ya upelelezi kuhusu mipango yake ya kutaka kutekeleza shambulio, kulingana na polisi.


    1 2 3 4 5 6 7
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako