• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (18 Machi-24 Machi)

    (GMT+08:00) 2017-03-24 18:08:57

    Aliyekuwa Makamu wa Rais wa DRC Jean-Pierre Bemba ahukumiwa kifungo cha mwaka mmoja kwa makosa ya kuhonga mashahidi

    Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jean-Pierre Bemba amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja kwa makosa ya kuhonga mashahidi.

    Tayari Bemba anatumikia kifungo cha miaka 18 kwa makosa ya uhalifu wa kivita kwa kuwatuma Wanajeshi wake kutekeleza mauaji katika nchi jirani ya Afrika ya Kati.

    Aidha akitoa hukumu hiyo jaji Bertram Schmitt ameagiza Bemba alipe faini ya dola $323 640.

    Majaji katika Mahakama hiyo wamebaini kuwa Bemba alitumia simu na lugha za siri kuwahonga mashahidi hao.

    Mahakama hiyo imesema hukumu hii itatoa funzo kwa na imetuma ujumbe kwa wale wote wanaozuia upatikanaji na haki katika Mahakama hiyo.

    Hii imekuwa ni kesi ya kwanza, kuhusu kuhongwa kwa mashahidi na kutolewa uamuzi na Mahakama hiyo yenye makao yake mjini Hague nchini Uholanzi.


    1 2 3 4 5 6 7
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako