• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (13 Mei-19 Mei)

    (GMT+08:00) 2017-05-19 18:48:43

    Shirika la afya duniani laonya kusambaa kwa Ebola DRC

    Shirika la afya duniani WHO wiki hii linaonya kuwa maambukizi ya Ebola Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, yanaweza kusambaa nchi nzima.

    Hadi sasa, watu 20 wamethibitishwa kuambukizwa ugonjwa huo hatari ambao tayari umesababisha vifo vya watu watatu katika mkoa wa Bas-Uele.

    Mapema wiki hii, WHO iliripotiwa kuwa watu 18 ndio waliokuwa wameambukizwa lakini idadi imeongeza na kufikia 20, hali ambayo imeanza kuzua wasiwasi katika eneo hilo.

    Mkurugenzi wa WHO anayehusika na maswala ya magonjwa ya dharura Peter Salama amesema kuwa ikiwa ugonjwa huo hautadhibitiwa mapema, huenda ukasambaa nchi nzima na hata eneo la Maziwa Makuu.

    Changamoto kubwa ya kuwafikia waathiriwa hao imeelezwa ni miundo mbinu mibaya kama barabara.

    Mara ya mwisho kwa Ebola kulikumba taifa hilo, ilikuwa ni mwaka 2014 na kusababisha watu 49 kupoteza maisha lakini baadaye maafisa wa afya wakafanikiwa kuudhibiti.

    Ugonjwa huu ulisumbua sana Mataifa ya Magharibi mwaka 2013 na kusababisha vifo vya watu 11,300 na kuwambukiza wengine nchini Guinea, Sierra Leone na Liberia.

    Dalili za Ebola ni pamoja na homa kali, kuumwa kwa misuli ya mwili, kuharisha, kutapika, kutokwa kwa damu kutoka maeneo yaliyo wazi ya mwili.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako