• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (13 Mei-19 Mei)

    (GMT+08:00) 2017-05-19 18:48:43

    Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa nchini Mali chashambuliwa tena

    Askari wanne wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Mali (MINUSMA)na askari watatu wa Mali wamejeruhiwa katika shambulizi dhidi ya kambi ya kikosi hicho mjini Tombouctou, nchini Mali.

    Ripoti iliyotolewa na Kikosi hicho imesema, wapiganaji wasiojulikana walirusha makombora manane katika kambi hiyo wakati wa hafla ya kumbukumbu ya miaka miwili tangu kusaini kwa makubaliano ya maridhiano na amani kati ya serikali ya Mali na upande wa upinzani.

    MINUSMA imelaani shambulizi hilo na kutoa wito kwa pande zote za makubaliano hayo kujitahidi zaidi kuhakikisha utekelezaji wa makubaliano hayo na kurejesha utulivu nchini humo.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako