• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (13 Mei-19 Mei)

    (GMT+08:00) 2017-05-19 18:48:43

    Wanajeshi waliokuwa wanagoma Cote Dvoire wamekubali kurudi kazini

    Wanajeshi waliokuwa wanagoma kwa siku nne nchini Cote Dvoire kushinikiza serikali kuwalipa marupurupu kama walivyoahidiwa mwaka 2010 hatimaye wamekubali kurudi kazini baada ya mwafaka kupatikana.

    Hatua hii imekuja baada ya serikali kuagiza kuwa wanajeshi hao walipwe marupurupu yao kila mmoja Euro 7,500 na salio linalobaki kulipwa ndani ya miezi miwili ijayo.

    Waziri wa Ulinzi nchini humo Alain-Richard Donwahi amethibitisha kuwa serikali imekubaliana na wanajeshi hao ambao tayari wamekubali kurudi kazini na kuondoka mitaani.

    Wanajeshi hao ambao zamani walikuwa ni waasi waliomsaidia rais Allasane Outtara kuingia madarakani mwaka 2010, waliahidiwa kulipwa Euro 18,000 kila mmoja kama malipo ya kumsaidia kiongozi huo wa sasa.

    Rais Outtara hata hivyo, amekuwa akiwasihi wanajeshi hao kuwa wavumilivu kwa sababu uchumi wa nchi yake unayumba kwa sababu ya kushuka kwa pato la zao la Cocoa.

    Wakati wa maandamano hayo, mtu mmoja alipoteza maisha, na zaidi ya wengine 10 kujeruhiwa kutokana na majeraha ya risasi katika katika jiji kuu la Abidjan na mji wa Bouke kulikofanyika maandamano hayo.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako