• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (21 Oktoba-27 Oktoba)

  (GMT+08:00) 2017-10-27 18:17:15

  Watu 10 wauawa katika mlipuko wa bomu la ardhini Somalia

  Watu wasiopungua 10 wameuawa na wengine zaidi ya 16 wamejeruhiwa baada ya msafara wa magari ya tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM kukanyaga bomu la kutegwa ardhini kusini ya Mogadishu.

  Ofisa wa usalama amesema tukio hilo limetokea katika eneo kati ya Arbiska na Lafole karibu na wilaya ya Afgoye, kilomita 30 kusini mwa Mogadishu.

  Msemaji wa vikosi vya AMISOM Bw Wilson Rono amethibitisha kwamba wahanga hao wameuawa katika mapambano kati ya vikosi vya Umoja wa Afrika na waasi wa Kundi la Al-Shabaab. Amesema askari mmoja wa AMISOM ameuawa na mwingine amejeruhiwa.

  Kundi la Al-Shabaab halijasema lolote kuhusu tukio hilo.

  Na nchini Kenya, Msemaji wa jeshi la Kenya KDF Bw. David Obonyo amesema, askari wa jeshi la Kenya wameshambulia kambi ya kundi la Al-Shabaab iliyoko huko Lamu na kuwaangamiza wapiganaji wanne wa kundi hilo.

  Amesema inaaminika kuwa magaidi kadhaa walikimbia wakiwa na majeraha. Kambi hiyo inadaiwa kutumiwa kama kituo cha mafunzo na kufanya operesheni cha magaidi, ambao wamefanya mashambulizi hivi karibuni katika eneo hilo nchini Kenya.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako