• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (18 Novemba-24 Novemba)

    (GMT+08:00) 2017-11-24 20:48:00

    Kikosi cha nne cha askari wa miguu wa kulinda amani wa China chaanza kutelekeza majukumu Sudan Kusini

    Batalioni ya nne na ya tatu ya askari wa miguu wa kulinda amani wa China nchini Sudan Kusini wiki hii zilifanya hafla ya kupokezana zamu katika kambi ya Umoja wa Mataifa huko Juba, kuashiria kuwa batalioni ya nne ya China imeanza rasmi kutekeleza majukumu yake nchini humo.

    Mkuu wa batalioni ya nne Bw Chen Ximing amesema operesheni za kulinda amani nje ya nchi ni jukumu kuu ililopewa na taifa, pia ni fursa ya kuonyesha sifa nzuri ya jeshi la China. Amesema batalioni yake itafanya juhudi zote katika kazi za kulinda amani nchini Sudan Kusini.

    Wakati huo huo ofisa wa Sudan Kusini amethibitisha kuwa mapambano yaliyoibuka tarehe 19 mwezi huu kati ya jeshi la serikali na kundi la waasi yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 25.

    Wakati huo huo nalo Jeshi la Uganda limetuma askari 106 kushiriki kwenye mazoezi ya wiki mbili ya kulinda amani ya Jeshi la Afrika mashariki EASF nchini Sudan.

    Msemaji wa jeshi la Uganda Brigedia Richard Karemire amesema kikosi hicho kinachoongozwa na Brigedia Michael Nyarwa kitashiriki kwenye mazoezi kwenye mji wa Port Sudan.

    Amesema mazoezi hayo yanayoshirikisha askari zaidi 1,000 kutoka nchi 10 za Afrika Mashariki, yatasaidia kuinua uwezo wa vikosi hivyo katika kulinda amani, kutatua mgogoro, na kupambana na ugaidi na magendo ya binadamu kwenye kanda hiyo.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako