• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (18 Novemba-24 Novemba)

    (GMT+08:00) 2017-11-24 20:48:00

    Dr Slaa aliyekuwa kiongozi wa upinzani ateuliwa kuwa balozi

    Aliyekuwa Katibu mkuu wa chama cha upinzani CHADEMA ameteuliwa kuwa balozi na Rais wa Tanzania, John Magufuli.

    Katika taarifa ilitolewa na Mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu ,Gerson Msigwa, haijataja kituo chake cha kazi. Ila imeeleza "ataapishwa baada ya taratibu kukamilika"

    Dokta Wilbord Slaa alikuwa kiongozi muandamizi wa upinzani nchini Tanzania.

    Alijiuzulu nafasi ya ukatibu mkuu na uanachama wa Chadema mwaka 2015 baada ya ujio wa waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa ambaye alipewa nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho mwaka huo.

    Slaa amekuwa katika siasa kwa zaidi ya miongo miwili na kabla ya hapo alikuwa padri wa kanisa katoliki.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako