• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (18 Novemba-24 Novemba)

    (GMT+08:00) 2017-11-24 20:48:00

    Rwanda yakubali kuwapokea wahamiaji 30,000 wa Afrika kutoka Libya

    Serikali ya Rwanda imesema iko tayari kupokea wakimbizi 30,000 wa Afrika kutoka Libya.

    Rwanda imejibu wito kutoka Umoja wa Afrika kufuatia suala la soko la watumwa nchini Libya.

    Waziri wa kigeni wa Rwanda Louise Mushikiwaboamesema amesema kutokana na falsafa ya kisiasa ya Rwanda na historia yao, hawawezi kusalia kimya wakati binadamu wanadhulumiwa haki yao wanateswa na kuuzwa.

    Louise Mushikiwabo alikua akijibu wito wa mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat, ambaye aliomba msaada kutoka nchi za bara la Afrika katika kukabiliana na hali hii nzito inayowakabili wahamiaji wa kiafrika.

    Rwanda inakuwa nchi ya kwanza kuitikia wito huu kwa kupendekeza kupokea wahamiaji 30,000 wa Afrika kutoka Libya.

    Habari kuhusu visa vya kuuzwa kwa wahamiaji kama watumwa ilifichuliwa na vyombo vya habari Novemba 14.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako