• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (25 Novemba-1 Desemba)

  (GMT+08:00) 2017-12-01 19:39:45

  Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya aapishwa

  Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ameapishwa kuiongoza nchi hiyo ya Afrika mashariki kwa muhula wa pili.

  Sherehe za kumwapisha rais Kenyatta na naibu wake William Ruto, zilifanyika katika Uwanja wa Kimataifa wa Michezo wa Kasarani katika mji mkuu Nairobi na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi.

  Marais na viongozi wa serikali kadhaa pia walifika huku usalama ukiimarishwa ndani na nje ya uwanja huo.

  Kwenye hotuba yake ya kuapishwa Rais uhuru Kenyatta anatoa wito kwa wenzake kwenye muungano wa upinzani NASA kujiunga naye ili kujenga taifa.

  Amesema atakuwa rais wa Wakenya wote, waliompigia kura na wale ambao hawakumpigia.

  Aidha ametangaza hatua kadhaa atakazochukua kwenye kipindi cha miaka mitano ijayo za kuboresha uchumi na maisha ya jamii kama vile kupunguza kwa asilimia 50 ada ya umme kwa watengenezaji bidhaa.

  Pia alitangaza kuwa raia wa jumuiya ya Afrika Mashriki, watahitaji tu kitambulisho kuingia nchini Kenya.

  Maris wageni wengine waliofika kwenye hafla hii ni, Paul Kagame wa Rwanda, Edgar Lungu wa Zambia, Ali Bongo wa Gabon waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn miongoni mwa wengine.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako