• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (15 Desemba-22 Desemba)

    (GMT+08:00) 2017-12-22 20:27:01

    Marekani yakosa kuungwa mkono na UN kuhusu swala la Israel

    Mkutano mkuu wa Umoja wa mataifa umepiga Kura ya kutoyatambua maamuzi ya Marekani ya kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

    Makubaliano hayo ya mkutano wa umoja wa mataifa yamefikiwa pamoja na vitisho vya Rais wa Marekani Donald Trump aliyetishia kuzikatia msaada wa kifedha nchi zote zitakazopinga msimamo wake.

    Mataifa mia moja ishirini wameyapigiakura maazimio, baadhi ya mataifa hayo yakiwamo washirika wa karibu wa marekani yaani Japan, Uingereza na Ujerumani.

    Canada na Mexico ni moja ya mataifa thelathini na tano ambayo hayakuhudhuria mkutano huo. Wapalestina wameiita hatua ya Umoja wa mataifa kuwa ni ushindi wa Palestina ingawa Israel imeyakataa matokeo.

    Kabla ya kura, balozi wa marekani katika umoja wa mataifa, Bi Nikki Haley alionya kuwa Marekani haitasahau au kusamehe pale nchi zilizoipinga Marekani zitakapokuja kuomba misaada.

    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako