• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (15 Desemba-22 Desemba)

    (GMT+08:00) 2017-12-22 20:27:01

    Mtoto wa dos Santos kwa tuhuma za ufisadi Angola

    Kampuni ya uma ya mafuta nchini Angola imetangaza kuanzisha uchunguzi kuhusu uwezekano kuwa kulikuwa na ubadhilifu wa fedha za shirika hilo uliofanywa na aliyekuwa mkurugenzi wake Isabel dos Santos, mtoto wa rais wa zamani wa nchi hiyo.

    Katika wiki za hivi karibuni vyombo kadhaa vya habari nchini Angola vimeripoti kuwa dos Santos aliagiza kuhamishwa na kulipwa kwa mamilioni ya fedha kinyume cha sheria.

    Dos Santos alichaguliwa na baba yake Jose Eduardo dos Santos mwaka 2016 kuwa mkurugenzi wa shirika la mafuta la uma na nafasi yake ilitenguliwa mwezi uliopita na rais mpya wa Angola Joao Lourenco.

    Isabel mwenyewe ameendelea kukanusha kuhusika na wizi au ubadhilifu wowote wakati akiwa mkurugenzi wa shirika hilo.

    Msemaji wa shirika la Sonangol, Mateus Benza amesema kuwa wameanzisha tume ya uchunguzi wa ndani na taarifa zitachapishwa.

    Kwa mujibu wa jarida la Novo Jornal na The Jornal Economico yameripoti kuwa Sonangol imebaini kuhamishwa kwa kiasi cha dola za Marekani milioni 67 kwenye akaunti ya Dubai.

    Wachunguzi pia wataangalia malipo ya kila mwezi yaliyoanzishwa baada ya Isabel kuingia madarakani, ambapo kampuni moja ya Ureno ilikuwa inalipwa kiasi cha Euro milioni 10.

    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako