• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (30 Desemba-5 Januari)

  (GMT+08:00) 2018-01-05 18:35:22

  Watu 12 wafariki kwenye ajali ya treni Afrika Kusini

  Treni ya kubeba abiria imeshika moto baada ya kugongana na lori nchini Afrika Kusini.

  Maafis awanasema watu 12 wamefariki na wengine 268 kujeruhiwa.

  Ukanda wa video umeonesha behewa moja la treni hiyo likiwa linawaka moja, pembeni kukiwa na gari lililopondwa pamoja na lori lililopinduka.

  Abira ambao waliokolewa kwenye treni hiyo walikuwa pembeni na mizigo yao wakiwa wamekwama.

  Ajali hiyo ilitokea karibu na mji wa Kroonstad katika jimbo la Free State baada ya lori kukosa kusimama katika makutano ya barabara na reli.

  Polisi wamenukuliwa wakisema abiria 850 wameondolewa kutoka kwenye treni hiyo wakiwa salama.

  Wizara ya uchukuzi ya Afrika kusini imeanzisha uchunguzi kuhusu ajali hiyo.

  Taarifa iliyotolewa na waziri wa uchukuzi wa Afrika kusini Bw. Joe Maswanganyi, inasema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa ajali ya treni kuacha reli ilisababishwa na lori lililojaribu kuvuka reli treni hiyo ya umeme iliwaka moto baada ya kugonga lori na kusababisha vifo na majeruhi.

  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako