• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (30 Desemba-5 Januari)

    (GMT+08:00) 2018-01-05 18:35:22

    Jeshi la Equatorial Guinea lasema lilizima jaribio la mapinduzi

    Jeshi la Equatorial Guinea limetangaza kwamba limefaulu kuzima jaribio la mapinduzi, baada ya kukabiliana na kundi la watu waliojihami kwa silaha za kivita kwenye mpaka na Cameroon.

    Katika taarifa iliyosomwa kupitia radio ya taifa, waziri wa ulinzi wa Equatorial Guinea, Nicholas Obama Nchama, aliwalaumu mamluki waliokuwa wamepewa kazi na makundi ya upinzani na kusaidiwa na mataifa ambayo hayakutajwa.

    Bw Nchama alisema kuwa mapinduzi hayo yalizimwa kwa msaada wa idara za usalama za Cameroon.

    Equatorial Guinea imeendelea kukumbwa na madai ya mapinduzi ya kijeshi.

    Kwa mujibu wa afisa mwandamizi wa serikali ya Equatorial Guinea ambaye hakutaka jinalake litajwe takriban watu 30 waliojihami kwa silaha za kivita kutoka Cameroon, Chad na Jamhuri ya Afrika ya kati walikamatwa mwezi uliopita kwenye mpaka nchini Cameroon.

    Kwa mujibu wa chanzo cha kijeshi, wanajeshi wa Equatorial Guinea walimuua kwa kumpiga risasi mamluki wakati wa makabiliano siku ya Jumatano Januri 3 karibu na mpaka na Cameroon.

    Serikali ya Rais Teodoro Obiang Nguema, imekuwa ikilaumiwa kwa ufisadi na ukiukaji wa haki za binadamu.

    Rais Teodoro Obiang Nguema amekuwa madarakani kwa karibu miaka 40, baada ya kuchukua madaraka kwa njia ya mapinduzi ya kijeshi mwaka 1979.

    Bw Obiang alimpindua madarakani mjomba wake Francisco Macias Nguema ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi.

    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako