• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (30 Desemba-5 Januari)

    (GMT+08:00) 2018-01-05 18:35:22

    Wapiga kura milioni 1.9 wajiandikisha kwa ajili ya uchaguzi Libya

    Tume ya uchaguzi ya Libya imetangaza kuwa hadi sasa idadi ya wapiga kura waliojiandikisha nchini humo imefikia milioni 1.9.

    Mwenyekiti wa tume hiyo Bw Emas Sayah amesema kazi ya uandikishaji ilianza tena mwezi uliopita, idadi ya wapiga kura waliojiandikisha katika mwezi huo imefikia laki 4, na kuifanya idadi ya jumla ya wapiga kura ifikie milioni 1.9 ikiwa ni pamoja na idadi ya awali ya milioni 1.5.

    Bw. Sayah ameongeza kuwa tume ya uchaguzi inataka kufikia lengo la kuandikisha wapiga kura milioni 2.5, pia ametaka idadi hiyo iendelee kuongezeka.

    Idadi hiyo ya wapiga kura itafanya kura za maoni na uchaguzi uaminike, na vyombo vitakavyoundwa baada ya uchaguzi huo vitatokana na maamuzi ya sehemu kubwa ya walibya. Tume ya uchaguzi inasubiri vyama vya kisiasa kufikia makubaliano kuhusu sheria ya uchaguzi, na sheria nyingine ya kura za maoni kuhusu rasimu ya katiba.

    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako